Tetesi zinasema, Manchester United, Tottenham na West Ham wanachuana kumsajili mlinda mlango wa West Brom Sam Johnstone, 28, msimu huu wa joto.

Mlinzi wa zamani wa England Sol Campbell ni miongoni mwa wale walioomba nafasi ya kuwa mbadala wa Aidy Boothroyd katika nafasi ya meneja wa kikosi cha England kwa wachezaji wa chini ya miaka 21.

Tetesi zinasema, Real Madrid wanamfuatilia mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling,26, ambaye anaweza kuondoka Etihad kwa kitita cha pauni milioni 75.

Tetesi zinasema, Kocha wa Everton Carlo Ancelotti anataka kumchukua mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 31, anayecheza kwa mkopo Tottenham msimu huu.

Tetesi zinasema, Chelsea wanaweza kujiunga na Manchester United na Liverpool kuwania saini ya winga Jadon Sancho baada ya Borussia Dortmund kushusha dau la kumnasa mchezaji huyo mwenye miaka 21 mpaka pauni milioni 85.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema Leeds United wanapenda kumsajili winga wa Club Bruge winga Mholanzi Noa Lang, 21.

Tetesi zinasema David Luiz, 34 anaingia miezi miwili ya mwisho ya kandarasi yake na Arsenal, wawakilishi wake wameanza kutafuta kilabu kipya kwa ajili ya Mbrazili huyo.

Kiungo wa kati wa Norwich City Emi Buendia, 24 anatolewa macho kwa kiasi kikubwa, huku Leeds United ikifikiria kumnyakua Muajentina huyo ambaye amehusishwa na taarifa za kutakiwa pia Arsenal, Aston Villa, Crystal Palace, Atletico Madrid, Sevilla na Villareal.

Rais wa zamani wa Inter Milan Massimo Moratti amemhimiza Narazzurri kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea, Mfaransa N’Golo Kante,30, kabla ya jaribio lao la kutetea taji la Italia msimu ujao.

Tetesi zinasema Borussia Dortumund inapenda kumsajili kiungo wa kati wa England Alex Oxlade-Chamberlain kutoka Liverpool msimu wa joto.

Barcelona imefanya mawasiliano ya awali na wawakilishi wa kiungo wa kati Gerson anayekipiga katika klabu ya Flamengo, wakati wakiangalia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo Mbrazili mwenye miaka 23.

 

Depay: Naweza Kubaki Lyon Mpaka Mwisho wa Msimu.

Tetesi zinasema mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay, 27, ana hamu kubwa ya kusainiwa Barcelona na tayari ameanza kutafuta nyumba katika jiji la Catalunya.

Massimiliano Allegri ameeleza nia yake ya kurejea kwenye uongozi wa mpira wa miguu na anahusishwa na taarifa za kurejea Juventus, wakati Real Madrid ikiwa kama chaguo jingine kwa Muitaliano huyo mwenye miaka 53.

Tetesi zinasema Roma na Inter Milan iko kwenye mapambano ya kupata saini ya kiungo wa kati wa Cagliari Nahitan Nandez, 25.

Tetesi zinasema Bayern Munich wanaongoza mbio za kumsajili kiungo wa kati Carney Chukwuemeka ,17,anayecheza klabu ya Aston Villa.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa