Tetesi za soka leo Ijumaa Mei 21, 2021 barani Ulaya zinasema:-

Tetesi zinasema, Mabingwa wa Ligi ya England Manchester City wamepania kumpa mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 26, mkataba mpya wa kudumu.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Real Madrid wa Wales Gareth Bale, 31, anaweza kuongeza muda wake wa mkopo na Tottenham kwa mwaka mwingine ikiwa Kane atapewa ruhusa ya kuondoka klabuni humo.

Tetesi zinasema, Manchester City wako tayari kuwashinda Manchester United na Chelsea kuipata sahihi ya mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 27 – ambaye anasisitiza Tottenham haiwezi kumzuia kuondoka.
Tetesi za soka -Bale
Tetesi zinasema, Wachezaji wa Spurs wanasemekana kushtushwa na uamuzi wa Kane kujitokeza kwa umma juu ya hamu yake ya kuondoka.

Tetesi zinasema, Kocha wa zamani wa Chelsea na kiungo wa kati wa England, Frank Lampard, mwenye umri wa miaka 42, amejiondoa kwenye harakati za kuchukua nafasi ya Roy Hodgson, 73, kama meneja wa Crystal Palace msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, Manchester United wako tayari kumsajili tena mlinda mlango wa Uingereza Tom Heaton mwenye umri wa miaka 35 kwa uhamisho wa bure kutoka Aston Villa. Mwingereza Sam Johnstone, 28, ambaye alikuwa mwingine aliyelengwa na na the Red Devils atahamia West Ham kutoka West Bromwich Albion.

Tetesi zinasema, Chelsea na Paris St-Germain wanafikiria kumchukua kiungo wa kati wa Bosnia mwenye umri wa miaka 31 Miralem Pjanic.
Tetesi za soka- Tom Heaton
Tetesi zinasema, Arsenal wameongeza juhudi zao za kumsajili kiungo wa Argentina mwenye umri wa miaka 24, Emiliano Buendia kutoka Norwich City inayoelekea ligi kuu wa England wakati the Gunners wakitaka kuziba nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Norway Martin Odegaard, 22, ambaye yuko tayari kurudi Real Madrid mwishoni mwa kipindi chake cha mkopo.

Tetesi zinasema, West Ham na Fulham wanaongoza harakati za kumsajili mshambuliaji wa Uingereza wa Blackburn Rovers, Adam Armstrong, ambaye thamani yake ni pauni milioni 25, lakini vilabu hivyo viwili vya London vinakabiliwa na ushindani kutoka kwa Brighton na Everton.

Tetesi zinasema, West Bromwich Albion iko tayari kuanza mazungumzo na bosi wa zamani wa Sheffield United Chris Wilder, 53, juu ya kuchukua nafasi ya meneja anayemaliza muda wake Sam Allardyce.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa