Kocha wa Aston Villa, Dean Smith anakusudia kukiimarisha kikosi chake katika safu ya ushambuliaji baada ya kufanikiwa kuepuka kushuka dara kutoka Premier League.

Katika kuhakikisha inafanikiwa katika hilo, wamekusudia kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, raia wa Ubelgiji Divock Origi, 25.

Tetesi za Usajili, Tetesi za Usajili, Meridianbet

Origi amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 44 pekee ndani ya Liverpool msimu huu uliyomalizika, lakini mara zote amekuwa mtu wa kusugua benchi akiwapisha Mo Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino wakianza.(Sun)

Mabingwa wa kombe la FA klabu ya Arsenal wanamlia rada beki wa kati raia wa Brazil, Diego Carlos huku Mikel Arteta akikusudia kukisuka upya kikosi chake kwaajili ya msimu ujao. (Telegraph)

Tetesi za Usajili, Tetesi za Usajili, Meridianbet
Arsenal inatarajia kutoa ofa nono kwa mshambuliaji wake raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang 31, wiki hii ya pauni milioni 250,000 kwa wiki katika makubaliano ya miaka mitatu kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo. (Mirror)

Tetesi za Usajili, Tetesi za Usajili, Meridianbet

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amepewa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 32, kuchukua nafasi ya Harry Kane kwa muda. (Mail)

Liverpool imeitangulia Paris St-Germain katika kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili Thiago Alcantara wa Bayern Munich na sasa hivi ina uwezekano mkubwa wa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania. (Mundo Deportivo, via talkSPORT)

Tetesi za Usajili, Tetesi za Usajili, Meridianbet

Mtendaji Mkuu wa Manchester United Ed Woodward amefanya mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji wa Lille Gabriel Magalhaes juu ya uhamisho wa mlinzi huyo wa Vrazil, 22. (RMC Sport, via Express)

Wakati huohuo, United inamatumaini ya kumtumia mlinzi Chris Smalling, 30, katika makubaliano ya mabadilishano na mlinzi wa Inter Milan, 25, raia wa Slovakia Milan Skriniar – lakini Roma inaendelea na machakato wake wa kumtafuta Mwingereza baada ya kuiridhisha timu hiyo alipokuwa kwa mkopo. (Star)


Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.

Ingia mchezoni

30 MAONI

  1. Habari njema hizi kwawale wa mchezaji ambao wako benchi kusajiliwa kwao inawapa fursa ya kwenda kuonyesha kuwa nao walikuwa bora kuwepo uwanjani pale walipo kosa nafasi hizo

  2. Hii ya aston villa hii na mashaka na forwald wetu mbwana samatta kukosa namba au kutolewa kwa mkopo baada ya kuonyesha kiwango kibovu pale villa park akija orig kutoka liverpool

  3. Binafsi naliangalia hili deal la Divock Origi kama ni ishara nzuri kwa Origi kwani atapata muda mwingi wa kucheza tofauti na anavyopewa Liverpool

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa