Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia miaka mitano Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kujishughulisha na mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa makosa ya kimaadili.

Mwakalebela pia ametozwa faini ya sh. 5,000,000 baada ya kutiwa hatiani kwa kutoa maneno ya uchochezi kwa nia ya kuchochea washabiki, wanachama na wapenzi wa Yanga dhidi ya vyombo vinavyosimamia mpira wa miguu nchini.

Fredrick mwakalebela.

Mwakalebela alilalamikiwa kuwa Februari 19 mwaka huu aliitisha Mkutano na Waandishi wa Habari na kudai kuwa TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi zinaihujumu timu ya Yanga, madai ambayo alishindwa kuthibitisha mbele ya Kamati.

Fredrick mwakalebela.

Katika shitaka Ia pili, Mwakalebela alilalamikiwa kwa kutoa taarifa za uongo ambapo Oktoba 1, 2020 aliitisha Mkutano na kudai kuwa anao mkataba kati ya mchezaji Bernard Morrison na klabu ya Simba na kuuonesha kwa Waandishi wa Habari huku akijua ni uongo na kitendo hicho ni kinyume na sheria.

Kamati imemtia hatiani katika shtaka hilo, na kumpa onyo la kutotenda kosa hilo kwa muda wa miaka mitano. Pia imemtoza faini ya sh. 2,000,000.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

mwakalebela, TFF Yamfungia Miaka Mitano Mwakalebela, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa