Beki wa Brazil, Thiago Silva anataka kusalia katika klabu ya Chelsea na yuko tayari kusaini mkataba wake mpya na The Bluez.

Chelsea iko tayari kutumia kifungu cha kuongeza mkataba wa Thiago Silva namchezaji pia anataka kubaki. Anangoja kuaini tu kwani anafurahi kubaki London.

Mkataba mpya hadi Juni 2022 bado haujasainiwa lakini pande hizo mbili zimefikia makubaliano ya maneno kuongeza muda huo.

Chelsea inatarajiwa kukamilisha maelezo ya mwisho na kusaini makubaliano hayo tu baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Thiago anathaminiwa sana ndani na nje ya uwanja kama ‘kiongozi wa kweli’ na amepanga kucheza Ulaya msimu ujao pia kwa sababu ya Kombe la Dunia huko Qatar mwakani.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa