Legendari wa soka, Thierry Henry ameweka wazi kuwa ni kweli anatambua mitandao ya kijamii kuwa na umuhimu mkubwa katika muingiliano wa watu na mambo mengine, lakini bado ameamua kujiondoa kwenye mitandao.

Mitandao ya kijamii kwa ujumla wake imekuwa ikilalamikiwa sana kwa unyanyasaji na ubaguzi, na kuwa hakuna njia mbadala iliyofaa kuzuia kabisa au kupunguza ubaguzi na unyanyasaji kupitia mitandao ya kijamii.

Thierry Henry amekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za watu wa rangi na jitihada za kutokomeza ubaguzi kwenye soka kwa ujumla. Henry anasema kuwa mitandao imekuwa sio sehemu salama na mamlaka zimeshindwa kuweka namna bora ya kuzuia vitendo vya ubaguzi.

Hata hivyo, mamlaka zinazohusika na mitandao mbali mbali zimeweka wazi nia yake ya kupambana na vitendo vya kibaguzi kwenye mitandao, Facebook wakiongoza jitihada kwa kuweka masharti yanayoboreshwa kadri muda unavyozidi kwenda ili kuendana na jitihada hizi. Facebook, kufuatia hili wametangaza kuzindua zana mpya ya kupambana na matukio ya namna hii.

Mitandao kama Facebook na Twitter, tayari inatoa mwanya kwa watumiaji kutoa ripoti ya viashiria vya matendo ya kibaguzi ya watumiaji wenzao wa mitandao. Na kumekuwa na visa kadhaa vya kufungwa kwa mitandao kwa watumiaji. Thierry anaungana na mastaa wengi wanaotumia mbinu tofauti kuleta mabdiliko katika jamii.


 

UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Thierry, Thierry Henry: Mitandao ya Kijamii Sio Salama, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa