Mshambuliaji nguli wa zamani wa Ufaransa na timu ya Arsenal, Thierry Henry aamua kujitoa kwenye mitandao ya kijamii rasmi mpaka pale ambapo maamuzi yatafanywa na wahusika.

Thierry Henry alizungumza hayo wakati akizungumza na BBC kuhusu kijitoa kwake katika mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ambapo unyanyasaji wa mtandaoni umekuwa ukiendelea.

Thierry Henry
Thierry Henry akipiga goti kipindi cha mechi (Getty Images)

“Ni wakati kuwa na msimamo” alisema Thierry Henry. “Nilihisi ni wakati wakuchukua maamuzi sahihi na kuwafanya wajue kwamba sio sawa kunyanyaswa mtandaoni, tumeona kukiwa na kesi nyingi za watu kujiua kutokana na mambo haya”, aliendelea.

Wakati huo huo mshambuliaji wa Totenham, Gareth Bale aliibuka juzi na kusema ataungana na wote wanaopinga manyanyaso ya mtandaoni baada ya wachezaji wenzake wa Wales kunyanyaswa.

Mchezaji wa Crystal Palace, Wilfred Zaha alisitisha kupiga goti hivi karibuni ikiwa ni jitihada za kuzuia unyanyasaji wa mtandaoni. Wilfred Zaha alisema “ifike wakati watu wasiwe wanaogopa kusoma maoni ya watu mtandaoni”

Kumekuwa na matukio mbalimbali ambapo wachezaji na wanasoka wamejaribu kuonyesha misimamo yao juu ya ubaguzi wa rangi mtandaoni. Huu ni wakati sahihi wa watu kuchukua maamuzi kuzuia mambo yanaweza kuleta matatizo makubwa duniani.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

thierry henry, Thierry Henry na Jitihada za kuzuia Ubaguzi wa rangi, Meridianbet

CHEZA HAPA

 

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa