Kuelekea mashindano ya Tokyo Olympics 2021, Andy Murray kuchuana na Felix Auger-Aliassime kwenye mzunguko wa kwanza kunako tenesi.

Murray ambaye anamedali 2 za dhahabu kwenye mashindano ya Olympic (2012 na 2016) alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kufanyia upasuaji marakadhaa.

Murray anakwenda kushiriki mashindano ya Tokyo Olympics akiwa ametoka kucheza Wimbledon 2021 pamoja na kupoteza mchezo dhidi ya Aliassime kwenye US Open 2020.

Kwa Aliassime, anakwenda kushiriki Olympics akiwa ametoka kwenye mashindano ya Wimbledon ambapo alimtoa Alexander Zverev kwenye hatua ya 16 na kufuzu hatua ya robo fainali.

Roger Federer, Rafael Nadal na Serena Williams ni miongoni mwa wachezaji wenye majina makubwa ambao hawatoshiriki mashindano ya Olympics huku mabingwa wa WimbledonNovak Djokovic na Ashleigh Barty wakiwa tayari wamewasili nchini Japan kuelekea kushiriki mashindano ya mwaka huu.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa