Mshambuliaji mdogo wa Manchester City, Ferran Torres alikuwa nyota wa mchezo wa jana baada ya kutupia hat-trick katika mechi iliyokuwa na magoli mengi kati yao na Newcastle United.

Katika mchezo ulionekana kuwa rahisi sana, City walilazimika kufanya kazi ya ziada ili kuhakikisha wanaondoka na ushindi katika mechi hiyo licha ya kuwakosa nyota wengi wa kikosi cha kwanza. Newcastle United walikuwa wa kwanza kufunga goli kabla ya mvua ya mabao kuanza.

Mwisho wa siku, dakika 90 zinakamilika na Ferran Torres anaibuka nyota kwa kufunga magoli matatu muhimu na kusaidia timu yake kuchukua ushindi muhimu ikiwa ni siku chache tu baada ya kutangazwa mabingwa.

Baada ya magoli hayo, Torres anatengeneza rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga magoli matatu katika timu ya Pep Guardiola. Akifanya huvyo hapo jana, akiwa na umri wa miaka 21 na siku 75 huku Messi alifanya hivyo mwaka 2010 akiwa na miaka 22 na siku 200.

Wengi wanaamini kuwa Ferran Torres anaweza kuwa mrithi wa Sergio Aguero endapo atapata muda mwingi wa kucheza.

Wakati huo huo kocha wa Man city Pep Guardiola amesema kuwa ameamua kumtumia mchezaji huyo ili kuwakumbusha wachezaji wa kikosi cha kwanza kuna kukosa kwa namba na inabidi wajiangalie nafasi zao.


Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Torres, Torres Atupia 3, Avunja Rekodi Ya Messi!, MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa