Thomas Tuchel amekuwa kocha wa kwanza kufikia fainali ya Eauropen Cup au Ligi ya Mabingwa mara mbili mfululizo na vilabu tofauti hakuna kocha aliyewahi kufanya hivyo.

Tuchel Aweka Historia Mpya Champions League

Chelsea ilifunga Real Madrid 2-0 siku ya Jumatano katika nusu fainali yao ya pili ya michuano hiyo na kukusanya jumla ya mabao 3-1 na sasa watakutana na Manchester City katika fainali.

Tuchel aliifikisha PSG fainali ya Champions League mwaka uliyopita na kuona timu yake ikicharazwa 1-0 na Bayern Munich.

Tuchel alisema: “Ninafuraha sana kwamba tumefanikiwa, nashukuru sana kupata fursa ya kuishi maisha ya soka kama taaluma yangu.

Chelsea kwa sasa wamefika fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya tatu na fainali zote wanakuwa wametoka kutimua makocha wao katikati ya msimu.

2007-08 walimtimua Mourinho na nafasi yake ilichukuliwa na Avram Grant ambaye aliifikisha fainali lakini ilishindwa na Manchester United kwa matuta.

2011-12 walimfungasha virago Andre Villas-Boas na mikoba yake ilichukuliwa na Roberto Di Matteo,ambaye alishinda kombe hilo dhidi ya Bayern Munich.

Historia imejirudia tena baada ya Tuchel kurithi mikoba kutoka kwa Frank Lampard mwezi Januari na Mjerumani huyo ameifikisha Chelsea fainali ya FA Cup na Champions League na kuisogeza mpaka nafasi ya nne kwenye ligi.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Tuchel, Tuchel Aweka Historia Mpya Champions League, Meridianbet

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa