Mashabiki wa Simba na wadau wa soka Tanzania na Afrika kwa ujumla bila shaka wanasubiri kwa hamu kuona kama Simba inaweza kurudia miujiza yao ya mwaka 1979 wakati itakapoikaribisha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika mechi ya marudiano ya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Jumamosi jioni.

Maajabu hayo ndio pekee yanayoweza kuiokoa Simba Jumamosi na kuiwezesha kukata tiketi ya kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo msimu huu baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini huko Afrika Kusini kwa mabao 4-0.

simba, Tunaweza Kuona Simba ya 1979, Meridianbet

 

 

Matokeo hayo yameifanya Simba kuhitajika kuibuka na ushindi wa kuanzia mabao 5-0 au zaidi ili waweze kusonga mbele vinginevyo wakipata idadi ya chini ya hayo watajikuta wakiaga na kushindwa kurudia kile walichokifanya mwaka 1974 walipofika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Lakini kumbukumbu ya kile ambacho Simba walikifanya mwaka 1979 dhidi ya Mufulila Wanderers ya Zambia, kinaweza kuleta tumaini kwa mashabiki wake kwamba wanaweza kupata ushindi mnono nyumbani ambao utawafanya watinge nusu fainali.

simba

Mwaka 1979, Simba licha ya kupoteza mchezo wa kwanza nyumbani wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mufulila Wanderers, ilifanya maajabu ugenini huko Lusaka Zambia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 ambao uliwafanya waingie raundi ya kwanza ya mashindano hayo.

Ukiondoa hilo, rekodi ya kufanya vizuri nyumbani katika mashindano ya kimataifa, inaweza kuwapa imani Simba ya kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Kaizer Chiefs kwani tangu walipofungwa mara ya mwisho uwanjani hapo na timu ya Recreativo Do Libolo ya Angola mwaka 2013 katika mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wamecheza jumla ya mechi 14 za mashindano ya klabu Afrika na wameibuka na ushindi mara 10, wamepata sare nne huku wakifunga mabao 32 na kufungwa mabao saba tu.

Mechi hiyo ya Jumamosi itachezeshwa na refa Pacifique Ndabihawenimana atakayasaidiwa na Emery Niyongabo na msaidizi namba mbili ni Pascal Ndimunzigo huku refa wa akiba akiwa ni Georges Gatogato ambao wote wanatoka Burundi.

simba, Tunaweza Kuona Simba ya 1979, Meridianbet
Pacifique Ndabihawenimana

Mechi nyingine za mashindano hayo mbali ya ile ya Simba na Kaizer Chiefs zitakuwa ni kati ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini itakayoikaribisha Al Ahly ya Misri, Wydad Casablanca ya Morocco itaialika MC Alger ya Algeria wakati Esperance ya Tunisia itacheza na CR Belouizdad ya Algeria.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa