Ikiwa ni baada ya masaa 24 tu yalipita tangu pambano la Tyson Fury na Anthony Joshua kuthibitishwa, mambo yamekuwa tofauti baada ya Deontay Wilder kuingilia kati mchakato.

Baada ya kutoka sare kwenye pambano la kwanza na Fury kushinda kwenye pambano la pili dhidi ya Wilder, kumeibuka taarifa kuwa pambano ya Fury vs Wilder kimkataba lilipaswa kuchezwa mara 3.

Kwa kuchezwa mara 2 pekee, Wilder anahaki ya kurejea ulingoni kuchuana na Tyson Fury kwa mara ya 3 wakipambania mkanda wa WBC ambao kwa sasa Fury ndio anaumiliki kama bingwa wa dunia baada ya kumzidi nguvu Wilder kwenye pambano lao la mizunguko 7.

Baada ya mazungumzo ya pande zote, Fury ameibuka na kusema kuwa Deontay Wilder anahitaji kulipwa pauni milioni 20 ili akae pembeni na kuruhusu Fury kupambana na AJ kumtafuta bingwa wa dunia.

Tyson Fury, Tyson Fury: Wilder Anataka Pauni Milioni 20., Meridianbet
Fury(kushoto) vs Wilder (kulia) kwenye pambano la kuwania ubingwa wa WBC.

Hata hivyo, tamko la Tyson Fury linapingwa vikali na mwalimu wa Wilder ambaye amesisitiza, wanachokitaka ni pambano lao la 3 ulingoni na sio suala la kupeana pesa. Kwa hali ilivyo, Fury hawezi kuchuana na AJ mpaka atakapomalizana na Wilder kama ilivyoamriwa na mahakama.

Kutokana na sekeseke hili, promota wa AJ, Eddie Hearn amenukuliwa akisema anafikiria kuangalia mipango mbadala ikiwa ni pamoja na pambano la lazima dhidi ya Oleksandr Usyk ambaye alipigwa na AJ kwenye pambano la kuwania mkanda wa WBO.

Tyson Fury, Tyson Fury: Wilder Anataka Pauni Milioni 20., Meridianbet
Usyk (kushoto) akichuana na AJ (kulia) katika pambano la kuwania ubingwa wa WBO

Pambano lililokuwa limepangwa kufanyika Agosti 14 kati ya AJ na Fury, lingempata bingwa wa dunia ambaye angeshinda mataji manne – WBO, WBC, IBF na WBA ambapo matatu anamiliki AJ na 1 analo Fury.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Tyson Fury, Tyson Fury: Wilder Anataka Pauni Milioni 20., MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa