Robert Lewandowski atakosa mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Paris Saint-Germain baada ya Bayern Munich kuthibitisha kuwa atakuwa nje kwa mwezi mmoja kutokana na jeraha la goti.
UCL: Lewandowski Kukosa Mechi Zote Dhidi ya PSG
Robert Lewandowski

Lewandowski alipata jeraha la goti lake la kulia wakati wa ushindi wa Poland wa 3-0 mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Andorra Jumapili, mchezo ambao alifunga mara mbili.

Awali ilifikiriwa kuwa mchezaji huyo wa miaka 32 angekuwepo tu kwa siku 10, hata hivyo, Bayern ilithibitisha siku ya Jumanne kuwa suala hilo ni kubwa kidogo kuliko ilivyotegemewa.

Taarifa iliwekwa wazi kwamba Lewandowski sasa anatarajiwa kuwa nje kwa mwezi Aprili.

Ilisomeka: “Robert Lewandowski amesumbua mshipa kwenye goti lake la kulia. Mshambuliaji huyo wa FC Bayern atakuwa nje kwa karibu wiki nne.

“Baada ya Poland kushinda 3-0 dhidi ya Andorra, Lewandowski alirudi mapema Munich, ambapo uchunguzi ulifanywa na timu ya matibabu ya mabingwa wa rekodi ya Ujerumani.”

Mabingwa hao wa Bundesliga wanakabiliana na wapinzani wao RB Leipzig wikendi hii, kabla ya kukutana na PSG katika Ligi ya Mabingwa.

Kukosekana kwa Lewandowski kutasababisha Bayern wasiwasi mkubwa katika ushambuliaji, na kikosi chao hakina mshambuliaji mwingine wa kati, ikimaanisha kuwa Thomas Muller atahamishwa kuchukua nafasi au Eric Maxim Choupo-Moting atachukua jukumu muhimu zaidi kwa sasa.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

Lewandowski, UCL: Lewandowski Kukosa Mechi Zote Dhidi ya PSG, Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa