Mabingwa wa ligi kuu ya Hispania klabu ya Real Madrid wameshatua kwenye jiji la Paris ndani ya uwanja wa ndege Charles de Gaulle international airport mishale ya saa 18:00 kwa majira ya Ufaransa baada ya kutumia masaa mawili angani.
Klabu ya Real Madrid watakaa kwenye hoteli ya Auberge du Jeu de Palme kwenye kitongoji cha Chantilly, kilomita 50 nje ya jiji la Paris. Kesho wanatarajia kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Stade de France na kufanya vikao na waandishi wa habari eneo hilo hapo kesho.

Kocha wa klabu hiyo Carlo Ancelotti ana kiskosi chake kamili kwa ajiri ya mchezo wa siku ya jumamosi, na mchezaji mwenye mashaka ya kucheza ni David Alaba, ambaye alikuwa na matatizo ya misuli. lakini amekuwa akifanya mazoezi na timu kwa wiki nzima pasipo tatizo lakini anatarajia kuwepo kwenye kikosi kitakacho anza.
Kikosi cha wachezaji 26 waliosafiri na timu ni.
Magolikipa: Thibaut Courtois, Andriy Lunin, Toni Fuidias.
Walinzi: Dani Carvajal, Eder Militao, David Alaba, Jesus Vallejo, Nacho, Marcelo, Ferland Mendy.
Viungo: Toni Kroos, Luka Modric, Casemiro, Fede Valverde, Lucas Vazquez, Dani Ceballos, Isco, Eduardo Camavinga.
Washambuliaji: Eden Hazard, Karim Benzema, Marco Asensio, Luka Jovic, Gareth Bale, Vinicius Junior, Rodrygo Goes, Mariano Diaz.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.