Mshambuliaji wa Klabu ya Rangers ya Scotland, Kemar Roofe amepigwa marufuku ya michezo minne na Mamlaka ya Udhibiti, Maadili na Nidhamu ya UEFA kwa kucheza Mchezo wa hatari kwa mchezaji mwingine.

UEFA pia Rangers imepiga faini ya euro 9,000 kwa vitendo viovu kwa Wachezaji wao wakati wa kipigo Chao huko Ibrox na faini inapaswa kulipwa ndani ya siku 90.

Marufuku hiyo ni kuendeleza kadi nyekundu ya Roofe kwa faulo mbaya kwa kipa wa Slavia Prague, Ondrej Kolar katika mchezo wa Europa League mnamo Machi 18.

 

uefa, UEFA Yamfungia Mechi 4 Kemar Roofe., Meridianbet

Kolar alitolewa na machela Siku hiyo na alivaa “head guard” wakati aliporudi uwanjani raundi inayofuata dhidi ya Arsenal, wakati Rangers mwishowe ilimaliza mechi na wachezaji tisa baada ya Leon Balogun pia kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Kutolewa kwao kwenye Europa League mwezi uliopita kuligubikwa na madai Glen Kamara alionyeshwa vitendo vya kibaguzi na Ondrej Kudela wa Slavia Prague, madai ambayo mchezaji na klabu walikanusha.

Kudela kapigwa marufuku ya michezo 10 baada kupatikana na hatia na UEFA, wakati Kamara pia Baada ya kuchunguzwa na baraza linalosimamia mpira wa miguu barani Ulaya akituhumiwa kwa shambulio katika tukio lililofuatia Baada ya filimbi ya mwisho, kapigwa marufuku ya Mechi tatu.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

uefa, UEFA Yamfungia Mechi 4 Kemar Roofe., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa