Wakati dunia ikiendelea kufurahia nusu fainali ya kombe la UEFA Champions League la wanaume na kushuhudia matokeo mbalimbali yasiyotegemewa, upande wa pili ligi hiyo hiyo kwa upande wa wanawake imeendelea kuboreshwa siku hadi siku kwa malengo ya kuifanya michuano iwe bora kama ile ya wanaume!

Kwanza kunatarajiwa kuwa na ongezeko la uwekezaji na kuongeza pesa kwa klabu zitazoshiriki mashindano hayo. Ongezeko hilo la pesa litalenga kuongeza kiwango cha zawadi zitakazotolewa kwa washindi na hata zile timu shiriki. UEFA pia imetazamia kuhakikisha kuwa ligi hiyo kwa upande wa wanawake inabaki kwa muda mrefu bila kupotea na uwepo wa pesa za kutosha ndio kitu pekee cha msingi.

Teknolojia ya Video Assistant Refereeing (VAR) ambayo ilikuwa inatumika fainali tu, sasa itatumika kuanzia robo fainali, lengo likiwa ni kupunguza kiwango cha utata wa maamuzi.

Jambo lingine lililoboreshwa ni kuruhusu timu kuwa na wachezaji wengi ambao wanaweza kuchukua nafasi za wale watakao na likizo za uzazi. Wale wachezaji vijana pia watakuwa na mtindo wa kuendelezwa vipaji vyao kwa utambulisho wa B-list ambao unahakikisha wachezaji wadogo wanaendeleza kuwepo.

UEFA pia imetangaza kuwa michuano hiyo inatagemewa kuanza kutimua vumbi rasmi Julai 28/29 baada ya droo ya kuchagua timu kufanyika tarehe 21 juni. Maboresho hayo yamelenga kuanza rasmi kwa mzunguko wa 2021-2025 yawe rasmi kabisa ili kuhakikisha burudani ya soka ya kutosha kabisa!

KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa