Shirikisho la soka ulaya, UEFA limesema litahakikisha linamfungia mchezaji au klabu yeyote itakayoshiriki kwenye European Super League. Hapo jana vilabu 12 vikubwa ulaya vilitangaza rasmi kuanzisha michuano hiyo kuanzia mwezi August mpaka May. Michuano hiyo imepangwa kufanyika nyumbani na ugenini.

Michuano hiyo ya European Super League itakuwa na jumla ya Timu 20 zitazotengeneza makundi mawili, kila moja likiwa na timu 10. Na watakaomaliza nafasi tatu za juu kila kundi watatinga robo fainali. Huku walioshika nafasi ya nne na tano katika makundi yote watapambana kutafuta mshindi mmoja wa kuungana nao robo fainali.

Klabu hizo zilieleza nia yao hiyo nzuri na kutaka kuzungumza na FIFA pamoja na UEFA lakini, taarifa rasmi kutoka UEFA zinasema zitafungia timu au klabu yeyote ambayo itashiriki mashindanpo hayo. FIFA nao wakaeleza kwamba kuanzishwa kwa mashindano hayo kutaondoa umoja na mshikamano kwani zitahusishwa timu kubwa tu huku zikiacha nyingine.

UEFA european super league

Timu tano kati ya 20 zitakuwa zinashuka kila mwaka na tano kupanda, vilabu vilivyoridhia kuunda michuano hiyo ni AC Milan, Inter, Juventus, Atletico, Barcelona, Real Madrid, Arsenal, Liverpool, Man City, Man Utd, Chelsea na Tottenham.

European Super League inaonekana kupingwa na watu wengi sana kutokana na sheria zake na ukweli kwamba zinabagua watu wengine. Sheria za michuano hiyo zinaeleza kwamba timu 15 anzilishi hazitashuka daraja. Kitu ambacho Klopp inaamini kinapoteza ladha ya mpira. “Hakuna mtu ambaye anatamani kuona Liverpool vs Real Madrid kwa miaka 16 mfulululizo” alisema Klopp alipoulizwa kuhusu maoni yake.

Je, katika suala hili UEFA na FIFA watakuwa sahihi au ni vilabu hivyo 12 vipo sahihi zaidi?

MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

european, European Super League Yazua Utata Duniani, Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa