Kocha wa klabu ya Tottenham Antonio Conte amesema kuwa ligi ya mabingwa ulaya inaweza kubadili maisha wakati ambapo klabu hiyi inapambana kutafuta nafasi ya nne ili ifanikiwe kucheza ligi ya mabingwa ulaya.

Kwa sasa klabu ya Tottenham ina alama tatu zaidi ya Arsenal ambayo inashika nafasi ya nne na alama sita dhidi ya West Ham na  Manchester United, huku Arsenal akiwa na mchezo mmoja mkononi.

Antonio Conte
Antonio Conte

Antonio Conte siku ya alhamisi alisema kuangalia ligi ya mabingwa ulaya kumeibua hali yake ya kutaka naye kushiriki.

“Arsenal, Man Utd, West Ham na Wolverhampton wote wako kwenye nafasi ya kuhitaji kushika nafasi ya nne, lakini tutapambana mpaka mwisho, na tutaangalia nini kitakacho tokea mwisho wa msimu. 

“Nadhani unajua vizuri mashindano ya ligi ya mabingwa kila klabu, kila mchezaji kila kocha anahitaji kucheza mashindano haya. 

“Kwa msimu huu ni muhimu kuwa na maono haya kwa sababu  inaweza kubadili maisha ikiwa msimu ujao tutakwenda kushiriki klabu bingwa badala ya kucheza Europa League, Conference League au kutokucheza mashindano yoyote ya aina hii.

‘Hali hii inatupa msukumo mkubwa na shauku kubwa ya kuamaliza nafasi ya juu kwa kadri tuwezavyo.” Alisema Antonio Conte


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa