Arsenal imefanikiwa kutinga fainali ya UEFA Champions League kwa mara ya pili katika historia ya klabu hiyo baada ya kuichapa Atletico Madrid kwa bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali, na kufuzu kwa jumla ya mabao 2-1. Ushindi huo umefika miaka 20 tangu walipocheza fainali yao ya kwanza.
Akizungumza baada ya mchezo, nyota wa Arsenal Bukayo Saka alisema “Ilikuwa ni mechi ngumu lakini tulijiamini tangu mwanzo. Mashabiki walituongeza nguvu na tulijua hii ilikuwa nafasi ya kihistoria.” Saka ndiye aliyefunga bao pekee la ushindi mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kipa Jan Oblak kuokoa shuti la Leandro Trossard.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa upande wa Atletico, mshambuliaji Julian Alvarez aliyekuwa na mashaka ya majeraha alikosa nafasi ya mapema, huku Giuliano Simeone akizuiwa na beki Declan Rice katika nafasi ya wazi. Kocha wa timu hiyo Diego Simeone alisema “Tulipambana sana lakini hatukutumia nafasi zetu. Arsenal walikuwa imara zaidi leo.”
Kipindi cha pili kilishuhudia Atletico wakiongeza presha ambapo Antoine Griezmann alilazimisha kipa David Raya kufanya save nzuri, huku Alexander Sorloth akikosa nafasi ya wazi mwishoni mwa mchezo iliyoweza kusawazisha.
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta alieleza furaha yake akisema “Hii ni hatua kubwa kwa klabu. Wachezaji wangu wameonyesha nidhamu na ubora wa hali ya juu. Sasa tunajiandaa kwa fainali.” Arsenal wameendelea kuwa hawajapoteza mchezo wowote katika mashindano hayo msimu huu.
Arsenal sasa watacheza fainali itakayofanyika Budapest Mei 30 dhidi ya mshindi kati ya Paris Saint-Germain au Bayern Munich, huku matumaini ya kubeba taji hilo kwa mara ya kwanza yakiwa juu kwa mashabiki wao.


