Kocha wa Arsenal FC, Mikel Arteta, amesema nahodha Martin Odegaard pamoja na mshambuliaji Kai Havertz wako tayari kucheza licha ya kukosekana kwenye mazoezi ya wazi kabla ya mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Atletico Madrid utakaopigwa katika dimba la Emirates.
Mchezo huo unakuja huku matokeo ya awali yakiwa 1-1, ambapo mabao yote yalitokana na penalti, Viktor Gyokeres akiifungia Arsenal na Julian Alvarez akiisawazishia Atletico Madrid. Hali hiyo inaacha kila timu ikiwa na nafasi sawa kuelekea mchezo wa marudiano.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza kabla ya mechi hiyo, Arteta alisema “Wote wako tayari, wapo kwenye kikosi. Hili ni jambo zuri kwa sababu tunahitaji chaguo na uwezo mpana wa wachezaji.” Aliongeza kuwa timu yake ipo tayari kupambana ili kufikia mafanikio makubwa barani Ulaya.
Arteta pia alionesha hamasa kubwa kuelekea mchezo huo akisema “Siwezi kusubiri. Nahisi nguvu kubwa ndani ya timu. Tumeweka juhudi kubwa kama klabu na kama kikosi, na huu ni usiku ambao watu wameusubiri kwa muda mrefu. Kitu cha ajabu kinaweza kutokea.”
Kwa upande wa Atletico Madrid, kocha Diego Simeone alisema wamebadilisha hoteli kabla ya mchezo huo jijini London, akisisitiza kuwa uamuzi huo ulikuwa wa gharama nafuu zaidi licha ya taarifa za vyombo vya habari kuhusisha na imani za kishirikina. “Sasa tuko vizuri zaidi kuliko tulivyokuwa Oktoba, na hoteli ni ya bei nafuu zaidi, ndiyo maana tulibadilisha,” alisema kwa utani.
Kuhusu hali ya kikosi, Simeone alithibitisha kuwa Alvarez, ambaye amehusika kwenye mabao mengi msimu huu, yupo kwenye kikosi licha ya kuwa na wasiwasi wa majeraha. “Julian ni muhimu katika mechi za aina hii. Anafahamu vizuri ligi na alicheza vizuri wiki iliyopita. Tunatumaini atafanya kile ambacho mchezo unahitaji,” aliongeza Simeone.


