Timu ya Atletico Madrid itacheza kwenye mchezo wake wa pili wa klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Manchester City leo usiku mbele ya mashabiki wao ambao wataujaza uwanja wote wa Wanda Metropolitano.

Awali Atletico Madrid walifungiwa na shirikisho la mpira barani ulaya UEFA kwa sababu ya mashabiki wake kufanya fujo kwenye uwanja wa Etihad, huku mmoja ya shabiki alionekana kurusha kitu kwenye uwanja wa Etihad.

Atletico Madrid walipinga kifungo ambacho UEFA walichowapatia cha kuacha viti 5000 wazi kwenye uwanja wao katika mchezo wa leo, Atletico waliwapaeleka UEFA kwenye mahakama ya CAS kuhusu sakata hilo, huku wakiwasilisha ombi lao kuwa ni ngumu kuwadhibiti mashabiki ambao tayari walikuwa washanunua tiketi zote kabla ya katazo hili kufanyika.

CAS wamekubali ombi la klabu ya Atletico na kuwataka UEFA kusitisha adhabu hiyo kwenye mchezo wa leo, na kuwataka kuwa adhabu hiyo itaanza kufanya kazi kwenye mchezo wa nusu fainali ikiwa watafanikiwa kufudhu au kwenye mchezo mwingine wa UEFA.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa