Shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya UEFA limeiadhibi klabu ya Atletico Madrid kwa kuwaagiza kuacha wazi sehemu za viti vya uwanja wake wa nyumbani kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa wa robo fainali siku ya jumatano dhidi ya Manchester City.

Adhabu hiyo imekuja baada ya mashabiki wa klabu ya Atletico Madrid kufanya fujo kwenye uwanja wa Etihad kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya ligi mabingwa Ulaya, ambapo kuna video iliyonyesha shabiki wa ATL Madrid akirusha kitu kwenye mchezo ambao Man city alishinda goli 1-0.

Atletico Madrid
Atletico Madrid

UEFA kupitia bodi yao ya kudhibiti maadili na nidhamu walitangaza kufanya uchunguzi wa jambo hilo siku ya ijumaa, leo jumatatu UEFA wamethibitisha kuiadhibu klabu ya Atletico Madrid kwa kuacha sehemu ya viti vya uwanja Wanda Metropolitano wazi kwenye mchezo kati yao na City.

Sehemu ya uwanja itafungwa siku ya jumatano kwenye mchezo wa marudiano, na klabu ya Atletico Madrid wameambiwa kuacha idadi ya siti 5000 wazi. UEFA kwenye waraka walioutoa ulisema kuwa wamewashurutisha ATL Madrid kutokana na tabia mbovu iliyonyeshwa na mashabiki wao.

Pia Madrid wanahitajika kuweka bango ambalo limeandikwa #NoToRacism kwenye mchezo wa siku ya jumatano.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa