Bayern Munich wametolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa marudiano uliopigwa mjini Munich, matokeo yaliyowapa PSG ushindi wa jumla wa mabao 6-5 na kufuzu fainali watakapokutana na Arsenal.
Nahodha wa Bayern, Manuel Neuer, amesema timu yake ilikosa “umakini wa mwisho wa kufunga mabao” jambo ambalo liligharimu nafasi yao ya kufika fainali. Bayern walichelewa kupata bao kupitia Harry Kane katika dakika za majeruhi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza, Neuer alisema “Hatukuwa na nafasi nyingi kubwa leo, lakini bado tulitengeneza za kutosha kufunga. Tulikosa ile hali ya kikatili ya PSG ya kutumia nafasi zao kufunga.”
Aliongeza kuwa bao lao lilikuja kuchelewa mno kuweza kubadilisha matokeo “Goli letu lilikuja muda umekwisha. Hatukuwa na muda wa kutengeneza nafasi nyingine au hata kupata mpira wa adhabu.”
Kocha wa Bayern, Vincent Kompany, alikubaliana na kauli ya nahodha wake lakini akasisitiza kuwa watajifunza kutokana na matokeo hayo. Alisema “Tulihitaji kuwa makini zaidi. Ni kipigo kigumu, lakini pia ni motisha kwa siku zijazo.”
Kwa matokeo hayo, ndoto ya Bayern kurejea fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu 2020 imefutika, huku PSG wakiendelea kuonyesha ubora wao katika michuano ya msimu huu.


