Mchezaji wa klabu ya Brentford na timu ya taifa ya Denmark Christian Eriksen ameshindwa kuficha furaha yake baada ya kufunga goli kwenye mchezo wake wa kwanza wa kimataifa japokuwa Denmark wamepoteza kwa goli 4-2 dhidi ya Uholanzi.
Christian Eriksen amekuwa nje ya uwanja kwenye michezo ya kimataifa kwa siku 287, baada ya kupata matatizo ya moyo katika mchezo wa ufungunzi kwenye kundi lao kwenye michuano ya Euro 2020.
Eriksen amefanikiwa kufunga kwenye mchezo huo ndani ya dakika mbili baada ya kuingia na kuishindwa kuizuia furaha yake pale alpohojiwa na alinukiliwa akisema, “najihisi kama mchezaji tena, nimekuwa nje ya uwanja kwenye michezo ya kimataifa kwa muda mrefu sana.
“Nina furaha kurudi tena, kufunikiwa kufunga imeniongezea furaha zaidi, inanipa hisia nzuri.
Ni vizuri nimefanikiwa kufunga, lakini ningeweza kufunga goli lingine la pili. Ni aibu mpira haukufanikiwa kuingia golini. Nilikuwa na miaka bora hapa na nakumbuka ambapo goli lilipo kwenye uwanja huu.”
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.