David Beckham Afichua Siri ya Mafanikio ya Luis Enrique PSG

Nyota wa zamani wa soka duniani David Beckham amefichua kile anachoamini kuwa kimeifanya mbinu za kocha Luis Enrique kufanikiwa ndani ya Paris Saint-Germain, baada ya klabu hiyo kufuzu fainali ya UEFA Champions League kwa mara ya pili ndani ya miaka miwili.

David Beckham Afichua Siri ya Mafanikio ya Luis Enrique PSGBeckham alisema baada ya PSG kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Bayern Munich, kuwa Enrique ameijenga timu yenye mshikamano mkubwa na nidhamu ya hali ya juu, jambo ambalo limeifanya PSG kuwa na ubora mkubwa msimu huu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akiwapongeza vijana wa PSG, Beckham alisema “Ni timu changa lakini yenye umoja mkubwa sana. Enrique amewajenga kuwa wachezaji wanaoelewana na kushirikiana kwa kila hali.”

David Beckham Afichua Siri ya Mafanikio ya Luis Enrique PSGBeckham pia alifichua kile alichosema kutoka kwa rais wa PSG kuhusu kocha huyo. Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi, alisema kuwa katika mwaka wake wa kwanza, Luis Enrique karibu kila siku alikuwa analala kwenye kituo cha mazoezi,” alisema Beckham.

David Beckham Afichua Siri ya Mafanikio ya Luis Enrique PSGAliendelea kueleza kujitoa kwa Enrique katika kazi yake ya ujenzi wa timu, akisema “Alikuwa akifanya kazi ya kuamua jinsi timu itacheza, nani anahitajika, na mustakabali wa timu unapaswa kuwa vipi.”

David Beckham Afichua Siri ya Mafanikio ya Luis Enrique PSGBeckham alihitimisha kwa kusema Enrique ameunda kikosi chenye nidhamu na malengo ya pamoja. Anataka wachezaji wote wafanye kazi kwa kiwango sawa, wawe na nia moja. Anawajenga vijana na anataka wachezaji wanaokimbia na wasiosimama. Hicho ndicho alichokijenga,” alisisitiza. PSG kwa sasa wanaongoza Ligue 1 kwa pointi sita na wanajiandaa kucheza fainali ya Champions League dhidi ya Arsenal mjini Budapest Mei 30.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.