Kocha wa PSG, Luis Enrique, amesema hana shaka na uwezo wa Arsenal baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, akimpongeza Mikel Arteta kwa kazi kubwa aliyoifanya tangu alipochukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo.
Akizungumza kuelekea fainali ya UEFA Champions League, Enrique alisema Arsenal na PSG zinafanana kwa namna nyingi licha ya kila timu kuwa na njia yake ya kufikia mafanikio ya msimu huu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha huyo wa Hispania alieleza kuwa PSG imefanya maandalizi ya kina kwa kuichambua Arsenal, timu ambayo wamekutana nayo mara kadhaa katika misimu ya hivi karibuni, huku akisisitiza kuwa fainali ni mchezo tofauti na mingine yote.

“Sioni kama kuna timu iliyo mbele ya nyingine. Arsenal na sisi tunalenga kitu kimoja, lakini tumefika hapa kupitia njia tofauti. Fainali huwa ngumu kila wakati, hivyo tutapaswa kutoa kila kitu tulichonacho huku tukifurahia mchezo huo,” alisema Enrique.

Akizungumzia kauli ya Arteta aliyesema Arsenal itakuwa mabingwa wa Ulaya, Enrique alisema PSG haihitaji motisha ya ziada kwani nafasi ya kushinda Champions League pekee inatosha kuwapa hamasa kubwa ya kupambana na kutetea heshima yao katika soka la Ulaya.


