Haaland,KDB, Messi Tatu bora Mchezaji Bora Ulaya

Wachezaji watatu waingia kwenye kinyang’anyro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa ulaya kwa mwaka 2023 ambao ni Earling Haaland, Kevin de Bruyne pamoja na Lionel Messi.

Wachezaji hao watatu wameingia kwenye orodha hiyo kutokana na ubora mkubwa ambao wamekua nao ndani ya mwaka 2023 na msimu uliomalizika ikiwa ndio sababu ya wao kuingia kwenye tatu bora ya kinyang’anyiro hicho.HAALANDMshambuliaji Earling Haaland alikua na msimu bora sana ambapo alifanikiwa kumaliza msimu akiwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uingereza na kuisaidia klabu yake kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja ikiwa ni rekodi kwa klabu hiyo.

Mchezaji Lionel Messi yeye alikua na mwaka wa mafanikio na akifanikiwa kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kutwaa ubingwa wa kombe la dunia akiwa na timu ya taifa ya Argentina, Mwaka 2022 alifanikiwa kuiwezesha timu yake ya taifa kutwaa ubingwa dunia huku akiwa mchezaji bora wa michuano hiyo.HAALANDKiungo Kevin de Bruyne yeye ni kama Haaland kwani yeye pia alikua mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Manchester City ambacho kilifanikiwa kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja, Huku yeye akionesha kiwango bora kabisa kwenye kikosi hicho na kumuwezesha kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Acha ujumbe