Kompany Asema Bayern Wanataka Historia Kuelekea Mechi Dhidi ya PSG

Kocha wa Bayern Munich, Vincent Kompany, amesema timu yake inajipanga kufanya tukio lisilosahaulika wakati watakapokutana na Paris Saint-Germain katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya UEFA Champions League.

Kompany Asema Bayern Wanataka Historia Kuelekea Mechi Dhidi ya PSG Bayern wanakabiliwa na kazi kubwa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 5-4, lakini Kompany amesema kikosi chake kimejaa imani kubwa. Alisema “Kuna hisia kwamba pamoja tunaweza kuchukua hatua inayofuata. Wachezaji na mashabiki wanaamini tunaweza kufika fainali.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo aliongeza kuwa Bayern wamepiga hatua kubwa msimu huu, akisema “Ni wachache waliamini mwanzoni mwa msimu kwamba tutakuwa na nafasi ya kufika hatua hii, lakini sasa tupo hapa na tunapambana hadi mwisho.”

Kompany Asema Bayern Wanataka Historia Kuelekea Mechi Dhidi ya PSG Pia alisisitiza utulivu ndani ya kikosi chake licha ya presha ya mchezo mkubwa, akisema “Utulivu wa hali ya juu, ndani ya timu kuna utulivu. Hatutaki mchezo huu ututawale mapema kichwani.”

Kompany Asema Bayern Wanataka Historia Kuelekea Mechi Dhidi ya PSG Kompany alieleza kuwa maandalizi yao yanalenga maamuzi madogo yatakayosaidia kupata ushindi, akisema Tunatafuta asilimia hiyo ya mwisho itakayotupa ushindi. Kipaumbele chetu ni kushinda mchezo.”

Kompany Asema Bayern Wanataka Historia Kuelekea Mechi Dhidi ya PSG Bayern tayari wameshinda taji la Bundesliga msimu huu na bado wana nafasi ya kutwaa mataji mawili, lakini macho yote sasa yameelekezwa kwenye mchezo huu muhimu wa Ulaya utakaofanyika nyumbani dhidi ya PSG.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.