Baada ya klabu ya Barcelona kumshushia kipigo cha paka mwizi timu ya Viktoria Plzen kwa goli tano moja kwenye mashindano ya klabu bingwa ulaya huku Lewandowski akifunga goli tatu peke yake.

Kiwango kizuri kilichoonyeshwa na Lewandowski dhidi ya Viktoria Plzen na kufanikiwa kufunga hat-trck alifanakiwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Lewandowski, Lewandowski Mchezaji Bora wa Ulaya wa Wiki, Meridianbet

Kwenye kura zilizopigwa wiki hii baada ya michezo ya klabu bingwa kuisha lewandowski amefanikiwa kuchukua nafasi ya kwanza, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Kylian Mbappe na ya tatu ikichukuliwa na Piotr Zielinski na ya nne Leroy Sane.

Hata hivyo bado ni mapema sana kuweza kuwatabiria wachezaji hawa kuwa nani ataweza kumudu mikimiki ya kila wiki kwenye usiku wa Ulaya na kuwa kwenye kiwango bora cha upachikaji wa mabao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa