Luis Enrique Afunguka Kabla ya Fainali ya UCL Dhidi ya Arsenal

Kocha Luis Enrique ameweka wazi mtazamo wake kuelekea fainali ya UEFA Champions League, ambapo Paris Saint-Germain itavaana na Arsenal. Enrique amesema licha ya kuheshimu uwezo wa Arsenal, hakuwa na hofu kubwa nao kama ilivyokuwa kwa Bayern Munich.

Luis Enrique Afunguka Kabla ya Fainali ya UCL Dhidi ya ArsenalAkizungumza na waandishi wa habari, Enrique alisema “Kama kuna timu niliyoogopa, ilikuwa FC Bayern Munich. Arsenal wamekuwa imara hivi karibuni, lakini kusema kweli, sijawahi kuwawazia sana.” Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki kuelekea mchezo huo mkubwa wa fainali.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

PSG ilitinga fainali baada ya kuiondoa Bayern Munich kwa jumla ya mabao 6-5. Katika mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa Mei 6, 2026, timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kwenye uwanja wa Allianz Arena, matokeo yaliyowapeleka PSG mbele kutokana na ushindi wa 5-4 walioupata Paris kwenye mkondo wa kwanza.

Luis Enrique Afunguka Kabla ya Fainali ya UCL Dhidi ya ArsenalKwa upande wa Arsenal, timu hiyo ilifuzu fainali baada ya kuiondoa Atlético Madrid kwa jumla ya mabao 2-1. Ushindi wa 1-0 kwenye uwanja wa Emirates kupitia bao la Bukayo Saka dakika ya 44 uliihakikishia nafasi ya kucheza fainali, baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza Madrid.

 

Luis Enrique Afunguka Kabla ya Fainali ya UCL Dhidi ya ArsenalEnrique pia alisisitiza kuwa PSG haitaingia uwanjani kwa mbinu za kujilinda. “Hatutakwenda kujilinda. Tunajua fainali inahitaji ujasiri na ubunifu. Tutacheza mpira wetu,” aliongeza kocha huyo.

Luis Enrique Afunguka Kabla ya Fainali ya UCL Dhidi ya ArsenalFainali hiyo ya UEFA Champions League inatarajiwa kuwa ya ushindani mkali kati ya timu mbili zenye uwezo mkubwa msimu huu, huku macho ya mashabiki duniani yakiwaelekea PSG na Arsenal katika pambano la kuwania ubingwa wa Ulaya.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.