Mateus Fernandes Azichanganya PSG na Manchester United

Klabu za Paris Saint-Germain na Manchester United zinatajwa kuwania saini ya kiungo wa West Ham United, Mateus Fernandes, huku klabu hiyo ikijiandaa kumuzaa nyota huyo katika dirisha lijalo la usajili.

Mateus Fernandes Azichanganya PSG na Manchester United West Ham ipo kwenye hatari ya kushuka daraja baada ya kubakiwa na michezo miwili ya mwisho ya msimu wakihitaji kufuta tofauti ya pointi mbili dhidi ya Tottenham Hotspur ili kujinusuru kutoka eneo la kushuka daraja.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika mchezo wao ujao, West Ham watasafiri kuwavaa Newcastle United kabla ya kuikaribisha Leeds United kwenye mchezo wa mwisho wa msimu. Endapo watapoteza dhidi ya Newcastle na Tottenham wakaifunga Chelsea FC, basi kushuka kwao kwenda Championship kunaweza kuthibitishwa mapema.

Mateus Fernandes Azichanganya PSG na Manchester United Ripoti kutoka The Athletic zimeeleza kuwa viongozi wa West Ham tayari “wanajiandaa kuishi bila Fernandes”, huku wakipanga kumuuza ili kupata fedha za usajili wa wachezaji wapya, bila kujali watabaki Ligi Kuu au watashuka daraja.

Mateus Fernandes Azichanganya PSG na Manchester United Fernandes mwenye umri wa miaka 21 ameonyesha kiwango bora tangu aliposajiliwa akitokea Southampton FC majira ya kiangazi yaliyopita. Kiungo huyo ameongeza mchango mkubwa baada ya kuondoka kwa Lucas Paqueta, akihusika kwenye mabao tisa katika michezo 40 msimu huu.

Mateus Fernandes Azichanganya PSG na Manchester United “Paris Saint-Germain na Manchester United zinafuatilia kwa karibu maendeleo ya Fernandes huku thamani yake ikipewa nafasi ya kuongezeka zaidi iwapo atafanya vizuri kwenye Kombe la Dunia akiwa na Ureno,” ilieleza sehemu ya ripoti hiyo.

Mateus Fernandes Azichanganya PSG na Manchester United
Fernandes kwa sasa anatajwa kuwa mmoja wa vipaji bora vijana katika Ligi Kuu England, jambo linalowafanya vigogo kadhaa wa Ulaya kuonyesha nia ya kutaka huduma yake kabla ya msimu mpya kuanza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.