Raisi wa zamani wa FIFA Sepp Blatter amekana kuwa malipo aliyothibitisha kulipwa raisi wa zamani wa UEFA Michel Platini haikuwa kinyume na sharia bali yalikuwa malipo halali  ambayo aliyaita “gentleman’s agreement” baina yao.

Mwendesha mashitaka wa mahakama ya Uswissi aliwashutumu wawili kwa kupanga njama ya kulipana kiasi cha  franc milioni mbili kinyume na sheria au kanuni za FIFA mwaka 2011. Lakini Blatter na Platini walikataaa mashitaka hayo.

Sepp Blatter, Sepp Blatter Akana Malipo ya Michel Platini, Meridianbet

Sepp Blatter alitoa maelezo kwenye mahakama ya makosa ya jinai jijini Bellinzona, baada ya kuomba hudhuru siku ya jumatano, kutokana na matatizo ya kiafaya. Blatter alieleza kuwa alimuomba Platini awe mshauri wake baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza FIFA mwaka 1998. Huku Platini akianza kazi rasmi mwaka 1999.

Platini aliomba alipwe francs milion moja kwa mwaka, lakini Blatter alimwambia kwamba FIFA haiwezi kumudu kiasi hicho cha mshahara, na badala yake wakakubalian kiasi francs 300,000 kwa mwaka, huku malipo hayo yakitarajiwa kulipwa baadae taasisi hiyo itakapo kuwa imara kiuchumi.

Blatter kwenye utetezi wake alisema, “nilipo fanya kazi na Platini nilijua kua tayari tumekubaliana mshahara francs 300,000 kwa kazi ya ushauri wa kifundi, tulishikana mikano kuonesha ishara ya  “gentleman’s agreement”.

Michel Platini wakati anahojiwa kwa nini hakuweza kudai pesa yake muda wote alijibu kuwa alikuwa anamuamini rais atamlipa wakati wowote, na aliposikia kuwa wafanyakazi wa FIFA wawili washalipa ndipo alipofanya mawasiliano akaambiwa apelekea invoice ya madai na alipopeleka ndani ya siku kumi alilipwa pesa yake.

Sepp Blatter na Michel Platini wote walizuiwa kujihusha na maswala ya soka kwa muda wa miaka sita, na ikiwa watakutwa na hatia basi wataadhibiwa kwa kwenda jela kwa kipindi kisichopungua miaka mitano.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa