Shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya wanaampango wa kuiwekea vikwazo Urusi ili kuizuia kuandaa michuano ya UEFA Euro 2028 baada ya kuwasilisha maombi ya kutaka kuanda michuano hiyo siku ya jumatano.
Kikao kilichofanywa na shirikisho la mpira wa miguu nchini Urusi moja ya dhima kubwa ilikuwa ni kuwasilisha maombi ya kuandaa mashindano ya UEFA Euro 2028 na 2032 kabla ya muda wa kusalisha maombi kufungwa.
Urusi waliingia kuomba ili kuweza kutoa changamoto kwa Uingereza na washirika ambao ilionekana kukosa mpinzani wa kuweza kushindana nao huku Uturuki nao wakiwa sehemu ya watu waliotuma maombi siku ya jumatano.
Italia naye alipeleka maombi ya kuandaa michuano hiyo mwaka 2032 ambapo Uturuki na Urusi nao wametuma maombi ya kuandaa kwa pamoja ikiwa watakosa nafasi ya kuandaa mashindano hayo mwaka 2028.
Chama cha soka nchini Urusi hakijawekewa vikwazo vyovyote na UEFA, licha ya kuwa timu zote za nchi hiyo za taifa na vilabu kuzuiliwa kushiriki michuano ya kimatiafa. Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu na mkurugenzi wa Gazprom Alexander Dyukov, bado mjumbe wa kamati kuu ya UEFA.
Kamati kuu ya UEFA iliseama “tunaweza kupitia maswala ya kisheria na ukweli uliopo kuhusu mambo yanayoendele na kuweza kuchukua maamuzi yatakayo hitajika, ikiwemo matamko mepesi ya urusi ya kutaka kuandaa michuano ya EURO”
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.