Shirikisho la mpira wa miguu barani UEFA limetoa sababu ya kuchelewa kwa mchezo wa fainali kwa dakika 35 siku ya jumamosi kati ya Liverpool dhidi ya Real Madrid huku klabu ya Liverpool wakitaka uchunguzi ufanyika kwa jinsi mashabiki wao walivyotendewa .

Mchezo ulipangwa kuanza saa 21:00 kwa majira ya nchini Ufaransa kwenye dimba la Stade de France jijini Paris na mchezo kusogezwa mpaka saa 21:36.

UEFA

UEFA walisema kuwa mchezo ulisogezwa mbele kwa sababu za kiusalama kutokana na msururu mkubwa wa mashabiki ambao hawakufanikiwa kuingia uwanjani.

“Kuelekea kwenye mchezo mlango wa kuingilia mashabiki wa liverpool ulifungwa ma mashabiki ambao walinunua tiketi za bandi kushindwa kusoma kwenye vifaa vya kielektroniki. Hii ilipelekea mashabiki kujikusanya na kutaka kuingia kwa nguvu.” Waraka wa UEFA ulisema.

Polisi wa jijini Ufaransa walitumia mtandao wa tweeter kuwataka mashabiki hao kutokulazimisha kuingia.

Pia baadhi ya mashabiki wenye tiketi halali nao walishindwa kuingia uwanjani hadi kwenye kipindi cha kwanza kinaisha ndipo walipopata nafasi ya kuingia. Kutokana na Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu ambao walianza kupanda uzio ili kuingia.

Klabu ya Liverpool imeomba uchunguzi ufanyike, huku wakiwaandikia waraka polisi uliosomeka, “PIcha isiyovutia kwenye mchezo, ambapo watu wa usalama walisambazwa uwanjani ili leta taharuki.

UEFA

“Nguvu ilitumika, wakati sehemu kubwa ya mashabiki hawakuonesha hali ya vurugu. Tumesikitishwa na tatizo lililotokea mlangoni na tatizo la ulinzi ambalo mashabiki wetu walikumbana jioni kwenye uwanja  Stade de France.

“Tumepeleka maombi rasmi kwa ajiri ya uchunguzikutokana na vitendo hivi visivyokubalika.”


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa