Hapa tunaongelea raundi 110! Wale kizazi kipya wanaweza kujiuliza inakaaje hii? Maana sasa hivi tunashuhudia mtu kalazwa chali ulingoni ndani ya sekunde kadhaa! Yaani anashindwa hata kumaliza dakika! Wakongwe wa mambo haya wanakwambia haujaona ndondi bado!

Ulingoni Masaa 7, Raundi 110!

Andy Bowen vs Jack Burke (1893)

April 6 mwaka 1893, Jack Burke na andy Bowen walipanda ulingoni na kupigana kwa raundi 110 pale Olympic Club, New Orleans . Pambano hili ndiyo pambano lililovunja rekodi ya kuwa pambano refu zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya ngumi za kulipwa. Rekodi ya mechi hii haijawahi vunjwa mpaka leo.

Pambano hili lilichukua masaa 7 na dakika 19, na zaidi ni kuwa hakuna mshindi aliyepatikana baada ya kumenyana kwa mda wote huo ulingoni. Muamuzi wa pambano hili ambaye alifahamika kama John Duffy alitangaza mechi kuwa sare, hivyo hakuna mshindi alipatikana kwa raundi zote.

Pambano la Masaa 7, Raundi 110 Katika Ndondi!

Pambano hili linatajwa kuwa lilikuwa na takribani mashabiki 8500 waliojitokeza kushuhudia pambano la lightweight. Bowen, bondia mzoefu alikuwa na uzito wa 129alitokea New Orleans. Mpinzani wake Burke kutokea Texas, ambaye alikuwa chipukizi wakati huo alikuwa na uzito wa 130.

Raundi zilikuwa na dakika 3, hadi kufikia ya 50, mabondia wote walianza kupunguza kasi ya kurushiana mikwaju ya nguvu.

Unaambiwa pambano hili lilikuwa gumu kutokea! Burke alivunjika viungio vya mikono lakini bado aliendelea kupambana. Walipokuwa kwenye raundi ya 51, Bowen alimuuliza mpinzani wake mbona alikuwa hajibu mapigo kwa kasi ya awali, akamjibu “Siwezi, mikono yangu yote imekwisha” Lakini jamaa hakuamua kushindwa pambano hili.

Licha ya Burke kuumia katika pambano, jamaa aliendelea kukaza hadi walipofika raundi ya 110 na muamuzi kuamua kuwa pambano limeisha, na ni sare! Pambano hili limebaki kwenye historia kama pambano lililopiganwa kwa mda mrefu zaidi!


KUWA SHUJAA KATIKA KASINO ZA MERIDIANBET!

SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

57 MAONI

  1. Mmh ilo pamabano lilikua gumu sana du muda wote uo walikua na mapafu ya dizain gan na pumzi ya kiasi gan duu hatar sana

  2. kwa sasa hakuna anaeweza kutimiza watu hawana upepo dakika kadhaa tu washafloat, kwakweli hiyo ilikua ni noma sana

  3. Sas Hawa watu wazamani kwel walikua miamba asa siwangeuwana na masaa 7 bado mnazichapa ujue baraa Hilo hahahahaa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa