Ukiniuliza mchezaji mwenye kipaji kikubwa zaidi Yanga, jibu langu litakuwa Tuisila Kisinda. Kasi kama ile ya Tuisila ni mtaji mkubwa sana kwa winga, haswa kwa timu inayoshambulia kupitia pembeni kama Yanga.

Lakini ukiniuliza mchezaji asiye na madhara kama inavotakiwa Yanga, jibu langu tena litakuwa Tuisila Kisinda. Ni mara chache sana utaiona hatari kwenye miguu ya Tuisila. Ni mara chache sana utaiona Yanga inanufaika na kasi ya TK. Shida ni nini?

Tuisila Kisinda
Tuisila Kisinda

Ninaweza kusema, timu haimsaidii kuwa hatari. Mara nyingi Yanga wanavocheza, wanamlazimisha Tuisila kuwa machachari badala ya kuwa hatari. Kama leo, Yanga walikuwa na mechi yao na Tuisila alikuwa na mechi yake tofauti.

Nadhani kocha na timu wanaweza kumsaidia zaidi Tuisila Kisinda kwa kumtega katika maeneo ya uwanja ambayo, atapata nafasi zaidi ya kushambulia kwa kasi. Kwa mfano Badala ya kumlazimisha kushambulia kwa kuingia katikati ambapo kuna idadi kubwa ya wachezaji anaweza kutengenezewa mazingira ya kwenda pembeni muda mwingi ambapo atapata nafasi ya kukimbia.

Lakini pia pasi ndefu za mabeki na zile za viungo kwenda kwake, anaweza kupigiwa kwa namma ambayo itakuwa rahisi kwake kushambulia na hatahitaji kufanya kazi nyingine ya ziada. Kwa mfano badala ya kumpiga pasi mguuni ambapo atahitaji kuwaacha mabeki kwanza, anaweza kupigiwa pasi mbele ya mabeki kisha majukumu yake yakaanzia hapo.

Tuisila Kisinda
Tuisila Kisinda

Lakini pia, nafikiri Tuisila sio mzuri sana mbele ya goli, hivo unaweza kumsaidia kwa kumchezesha kwa namna ambayo atakupatia magoli kwa kutoa assist au semi-assist badala ya kumpa jukumu zito la kufunga ambalo sio mzuri sana.

Bado ninaamini Tuisila ni mchezaji mwenye talanta kubwa ambayo timu na kocha wakiamua kumsaidia atakuwa mchezaji hatari zaidi Yanga. Naomba kuwasilisha mheshimiwa


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Tuisila Kisinda, Umuhimu wa Tuisila Kisinda Pale Jangwani, MeridianbetBASHIRI SASA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa