McGregor alijipindua na kumletea ubabe shabiki wake!

Mpiganaji wa ndondi mchanganyiko McGregor aliwekwa kizuizini na na polisi wa America Machi 2020 baada ya kuripotiwa kuwa alipokonya na kuivunja kwa makusudi simu ya shabiki nje ya klabu ya usiku kule Florida.

Mpiganaji huyu alikuwa na shtaka la unyanganyi wa kutumia nguvu baada ya kuchukua simu hiyo ya shabiki na kuipasua. Polisi wa Miami walidai kuwa waliitwa eneo la tukio mida ya saa kumi na moja asubuhi nje ya klabu ya usiku ya LIV.

Baada ya kuanza uchunguzi McGregor alikamatwa na kuwekwa kizuizini Miami-Dade. Dhamana yake iliwekwa kwa $12 500

Kwa mujibu wa ripoti, shabiki ambaye simu yake ilipokonywa na alijaribu kumpiga picha McGregor kwa simu yake ambayo inatajwa kuwa na thamani ya $1 000 (sawa na TSH2,319,114). Baada ya maywether, kuichukua simu hiyo na kudua juu yake, aliondoka nayo bila kuirudisha.

Kamera zilizotegwa maeneo ya kumbi hiyo zilimnasa McGregor akifanya tukio hilo. Shabiki alisimulia kuwa McGregor aliitandika ngumi simu yake, aliihisi ngumi ile kwenye mwili wake.

Shabiki alipotaka kichukua simu yake ambayo ilikuwa imedondoka, Mcgregor akaichukua yeye na kuibamiza tena chini kabla hajaikanyaga kama mara 4 kisha akatokomea zake na simu.

Huyu jamaa, ni mwanandondi ambaye hupenda kufanya mazali ya rejareja, alishawahi kuvamia basi lililokuwa na wapinzani wake kadhaa na kuwatupia chuma, kosa lililomuacha na adhabu ya kifungo cha nje na adhabu ya kupata mafunzo ya kuzuia hasira.


 

Kuna ofa kibao unazofaidi ikiwa unabashiri na Meridianbet. Jiunge sasa kufurahia ofa zetu

Bonyeza HAPA Kujiunga.

33 MAONI

  1. Labda alihisi anamudhihaki baada ya kupigwa na Floyd Mayweather . Inasikitisha mtu anapokuwa public figure anafanya vituko visivyoelezeka kirahisi#meridianbettz

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa