Wakati Man United wakiendeleza jitihada zao za kuimarisha kikosi chao hasa eneo la ushambuliaji, jina la Andre Silva limeibuka kama moja ya malengo ya klabu hiyo.

Andre Silva amekuja kama moja ya malengo hayo baada ya usajili wa Erling Haaland kuonekana kuwa mgumu, baada ya nyota huyo wa Borussia kutaja dau la mshahara mkubwa wa wiki endapo atasajiliwa klabuni hapo. 

Silva anakipiga katika klabu ya Frankfurt, mpaka sasa ana magoli 23 katika michezo 26 aliyocheza ya Bundesliga, akiwa nyuma ya Lewandowski mwenye magoli 35. Silva amempiku Haaland mwenye magoli 21.

Dau lililotajwa kwa Silva ni Euro milioni 40 tu! Tofauti na Haaland ambaye aliwekewa kiasi cha Euro milioni 180 na mshahara mkubwa mno. Andre Silva anaweza kuwa ingizo muhimu sana endapo tu Solskjaer na Edi Woodward wataamua kufanya usajili huo.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

andre silva, United: Andre Silva Kuwa Mbadala Wa Haaland?, Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa