Cristiano Ronaldo anaripotiwa kuwa hatajiunga tena na Manchester United wakati wa msimu huu wa usajili wa majira ya joto kwani mabingwa hao wa mara 20 wa Uingereza hawawezi kumsajili mshambuliaji huyo wa Juventus.

Hatma ya staa huyo wa Ureno huko Turin kwa sasa ipo mashakani wakati kuna maoni kwamba anazidi kuchanganyikiwa na maisha katika klabu yake ya sasa Italia.

Kurejea Man United kulitajwa kuwepo katika uwezekano wa mpango wa uhamisho, na Mashetani Wekundu wakidhaniwa wako tayari na wazo la kumrudisha Old Trafford nyota wao wa zamani mwenye umri wa miaka 36 katika soko lijalo.

Ronaldo Juventus

Hata hivyo, kwa mujibu wa na Sport Mediaset, upande wa Ole Gunnar Solskjaer hautaweza kumudu dau la jumla la Ronaldo, ambaye anaaminika kulipwa Pauni 540,000 kwa wiki huko Turin, wakati Bibi Kizee akidaiwa atahitaji ada kubwa ya uhamisho msimu huu wa joto.

Ripoti hiyo inadai kwamba Mreno huyo anajiandaa kuona mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa Juve kabla ya kutafuta klabu nyingine mwishoni mwa kampeni ya 2021-22.

Ronaldo, ambaye amefunga mabao 34 katika mechi 40 kwa kikosi cha Andrea Pirlo msimu huu, pia kwa sasa anahusishwa na kurudi Sporting Lisbon.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Ronaldo, United Hawataweza Kumrejesha Ronaldo, Meridianbet

SOMA ZAIDI

9 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa