Timu ya Manchester United imeripotiwa kuwa ipo tayari kutoa Euro milioni 50 kwa ajili ya kupata saini ya mchezaji wa Barcelona, Ousman Dembele katika malengo ya kuboresha eneo la ushambuliaji.

Kutoka kwenye jarida la Fichajes la Spain, Barcelona wameweka dau la euro milioni 50 kwa mchezaji huyo kama klabu hiyo ya Uingereza watahitaji huduma ya Dembele.

United wamekuwa mawindoni kutafuta mshambuliaji wa kudumu wa klabu hiyo baada ya mkataba wa mchezaji wao wa sasa Edinson Cavani kuelekea ukingoni huku mchezaji huyo akisuasua kuongeza mkataba.

Mchezaji huyo wa Ufaransa amekuwa na msimu mzuri katika kikosi cha Koeman cha msimu huu akifunga magoli 10 na kutoa pasi za magoli 4 kwa michezo 39 ya mashindano yote aliyochezea klabu ya Barcelona.

Kutokana na hali mbaya ya uchumi ya Barcelona na mchezo usiokuwa bora wa mara kwa mara, wanalazimika kumuuza mchezaji huyo ili kuweza kuboresha kikosi chao kwa msimu ujao baada ya watu muhimu kama Lionel Messi kutangaza nia ya kutimka klabuni hapo akiwa amebakiza miezi miwili tu kwenye mkataba wake na klabu ya Barcelona.

United wamekuwa wakitafuta saini ya mchezaji huyo wa Barcelona toka msimu uliopita bila mafanikio, huku ule usajili mkubwa wa Jadon Sancho wa Dortmund nao ukionekana kutoonesha mafanikio yoyote!

KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa