Klabu ya Manchester United imeripotiwa kuwa imefanya mazungumzo na Edinson Cavani wakijaribu kumshawishi staa huyo kusalia hata baada ya msimu huu.

Hatma ya nyota huyu mwenye miaka 34 ilikuwa na sintofahamu baada ya baba yake kuweka wazi kuwa mwanaye hajihisi kuwa huru pale Uingereza. Kocha msaidizi wa Uruguay, Mario Rebollo pia aliongeza uzito kwenye suala la nyota huyu kuondoka aliposema ni vyema akaenda mahali pengine kutafuta ushindani zaidi.

Edinson Cavani United
Kwa mujibu wa Daily Mail, mkurugenzi mpya wa United John Murtough, pamoja na makamu mwenyekiti Ed Woodward wamekutana na Cavani jumanne na kuzungumza naye ikiwa ataongeza mwaka mwingine kwenye mkataba wake.

Mshambuliaji huyu wa zamani wa Paris Saint-Germain na Napoli anatambua kuwa kipaumbele cha Ole Gunnar ni kusajili mchezaji mwingine kwa nafasi yake, na kwa sasa anafikiria zaidi kuhusu idadi ya mechi ambayo atakuwa anaipata.

Cavani amecheza mechi 26 msimu huu na kuwafungia mashetani wekundu magoli saba na kutoa asisti mbili.


 

UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

United, United Wafanya Mazungumzo na Edinson Cavani, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa