Manchester United wanajiandaa kuelekea kuchuana na klabu ya Leicester City Jumamosi. Kikosi cha Ole Gunnar mpaka sasa kina majeruhi 8, majeruhi ambao wanaweza kuathiri harakati za kutafuta ushindi dhidi ya Leicester.

Mashetani Wekundu kwa sasa wamekalia nafasi ya nane kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya kutokuanza vyema sana msimu huu. Hata hivyo, Man U bado wana nafasi ya kurejesha bahati yao njema wakiwa wenyeji wa Leicester wikiendi hii.

Kuelekea mechi hii hofu ipo kwenye idadi ya majeruhi walionao. Mastaa kadhaa wana shida ya majeraha ambao ni Timothy Fosu-Mensah na Eric Bertrand Bailly wanaosumbuliwa na majeraha ya goti, Luke Shaw, Diogo Dalot na Anthony Martial wanasumbuliwa na paja, wakati Paul Pogba akisumbuliwa na enka, pia Aaron Wan-Bissaka yeye akisumbuliwa na mgongo huku Jesse Lingard akibanwa na homa.

United wanaweza kuwa na mipango ya kufanya vyema zaidi ili waweze kujiweka katika nafasi nzuri. Kwao watakuwa na nafuu ya kuwepo nyumbani, ikiwa baadhi ya mastaa wao watarejea kuwa na hali nzuri na itakuwa nafuu zaidi kwa Man United.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa