Mchezo wa La Liga kati ya Valencia na Cadiz, ulisimamishwa kwa muda baada ya timu ya Valencia kutoka nje uwanja baada ya beki wao Kisiki Mouctar Diakhaby kuambiwa maneno ya kibaguzi na mchezaji wa Cadiz Juan Cala.

Katika mechi hiyo Diakhaby alionekana kukasirishwa baada ya kugongana na Juan Cala wakati wa jitihada za kuwania mpira. Diakhaby aliwaambia wachezaji wenzake kwamba alisikia maneno ya kibaguzi kutoka kwa mchezaji huyo na maneno ambayo hawezi hata kuyataja.

Baada ya kukaa nje kwa muda, Valencia waliamua kurudi uwanjani baada ya beki huyo kuwaambia warudi uwanjani ili wasipoteze mechi hiyo. Licha ya Valencia kurudi uwanjani beki wao hakuweza kuendelea na mchezo huo kutokana na kujisikia vibaya baada ya kitendo hicho.

Mouctar Diakhaby wa valencia
Mouctar Diakhaby akiongea na mwamuzi kabla ya wao kutoka nje ya uwanja
Nahodha wa Valencia alisema wanaamini katika usawa na kitendo alichofanyiwa mwenzao si cha kiungwana na ni lazima kikemewe na wao baada ya kuambiwa mwenzao kafanyiwa hivyo wakalazimika kutoka.

Lakini licha ya Valencia kurudi uwanjani kupambania alama zao tatu, waliambulia kipigo cha bao 2-1 dhidi ya wapinzani wao Cadiz.

Cadiz pia walisema timu yao inapinga vikali vitendo vya ubaguzi wa rangi na wanaamini kwamba wachezaji wao wapo timamu na ni mabalozi wakubwa katika kuzuia ubaguzi wa aina yoyote ile.

Kwa sasa dunia imekuwa ikikumbwa na majanga mengi ya ubaguzi wa rangi kwenye michezo mbalimbali hasa mpira wa miguu, je ni kwamba ubinadamu umefika kikomo na rangi ya mtu inatawala?


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa