Ligi kuu Tanzania bara, VPL, Iliendelea hapo jana ambapo vijana wa Dodoma Jiji waliwaalika matajiri wa Dar es salaam, Azam FC na kuwalazimisha sare ya 2-2, katika mbio za kuwania top 4 ya VPL.

Vita hiyo ya kuwania nafasi nne za juu za VPL imeshika kasi sana mzunguko huu wa pili wa ligi ambapo kila timu inaonekana kutupia jicho nafasi hizo za juu. Katika mbio hizo timu ambazo zimeongoza chachu ya ushindani ni Biashara United, KMC, Dodoma Jiji pamoja na Ruvu Shooting.

Awali VPL, ilikuwa ikitawaliwa sana sana na vilabu vya Simba, Yanga na Azam lakini msimu huu mambo yamekuwa magumu, kwani timu hizo nne hapo juu zinakuja kwa kasi ya kimbunga jobo!

Biashara United wanashika nafasi ya nne wakiwa na alama 41, KMC wapo nafasi ya tano wakiwa na alama 40, Dodoma Jiji nafasi ya 6 wakiwa na alama 38 huku vijana wa Bwire wakiwa na alama 37 katika nafasi ya 7.

Kutokana na fununu zilizopo kuwa kuwa uwezekano wa Tanzania kutoa timu nne kwenye michuano ya Afrika kutokana na timu ya simba kujikusanyia alama nyingi katika CAFCL.

Katika kinyang’anyiro cha ubingwa wa VPL, vita bado ni kubwa kati ya vigogo wa soka pale juu, ambapo Wekundu wa Msimbazi wanaendelea kumfukuzia mwizi kimya kimya wakitaka kurejea kileleni baada ya kuwa na viporo vya mechi 3.

Wikiendi hii, kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kati ya Yanga na Azam siku ya jumapili majira ya saa 2.15 usiku, wakati Simba watakuwa kule Mwanza kupepetana na Gwambina siku ya jumamosi.

Kumbuka kuwa Yanga inaongoza ligi ikiwa na alama 57 huku Simba ikiwa nafasi ya pili na alama 55 wakiwa na michezo mitatu mkononi. Endapo Simba itashinda mechi ya kesho dhidi ya Gwambina itarejea juu, lakini kama Yanga itapata ushindi basi itarudi… Kimsingi ni kwamba Kimeumana VPL msimu huu!


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

VPL, Vita ya Top 4 VPL, Ataachwa Mtu, Meridianbet

CHEZA HAPA

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa