Wakala wa mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann ameripotiwa kufanya mazungumzo na timu za Ligi Kuu wakati kukiwa na uvumi kuhusu sintofahamu ya hatua anayoenda kuichukua ya Mfaransa huyo.

Pamoja na Barcelona kuwa chini ya shinikizo kubwa la kupunguza mzigo wamatumizi ya fedha kwenye dirisha la sasa, Griezmann anaeleweka kuwa moja ya majina kadhaa yaliyowekwa kwenye mpango wa kupunguza wachezaji.

Wakala wa Griezmann Awasiliana na Timu za EPL

Atletico Madrid wamehusishwa sana na mshambuliaji wao wa zamani kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana yanayomuhusu Sauli Niguez, lakini hakuna ushahidi kuwa kuna makubaliano yoyote juu ya pendekezo kama hilo

Chelsea wanahusishwa na nia ya kumchukua Griezmann kwa mkopo, wakati Manchester City, Liverpool, Juventus, Paris Saint-Germain na Bayern Munich zote zikitajwa kuwa windoni dhidi ya saini ya staa huyu, lakini Atletico bado wanaendelea kuongoza orodha hiyo.

Barcelona wanatajwa kusita kufanya maamuzi juu ya hatma ya Griezmann, ambaye amejitahidi sana akiwa na Barcelona, akiwa na idadi nzuri ya mabao 20 na asisti 13 kwenye michezo 51 ya mashindano yote msimu uliopita.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa