Brazil ni taifa ambalo linauishi mpira na kuonesha uwezo wao wa kuuchezea mpira na kwamba wana kila linaloonekana kithibitisha kwamba wamejaliwa kwa namna moja au nyingine kuweza kuweka historia ndani ya mchezo huo. Kwa taifa hilo mchezaji wao yoyote ana heshima kubwa na hupewa heshima yake kutokana na mchango wake anaoutoa ndani ya timu yao. Pamoja na masuala ya kisiasa yanayolisumbua taifa hilo lakini bado wamebaki imara kwenye soka. Naadhi ya nyota waliosumbua sana katika taifa hilo:

Pelé

Pamoja na kuzidiwa na wachezaji kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo katika rekodi zake ndani ya soka, mchezaji huyo bado amebaki kuwa kioo cha wachezaji wengi wanaokua kisoka ndani ya taifa hilo na nje, kwa kuacha historia ambayo kwa namna moja au nyingine. Jambo hilo limeweza kuchangia kwa namna fulani kuweza kupata heshima kubwa. Alianza kugonga vichwa vya habari baada ya kushinda kombe la dunia mwaka 1958 akiwa na miaka 17.

Ronaldo de Lima

Pamoja na kuwa na majina hayo mawili yenye historia kubwa barani Ulaya, lakini kuna Ronaldo mmoja tu ambaye amekuwa gumzo sana miaka ya nyuma kutokana na uwezo wake wa kufunga wakati wowote ndani ya taifa hilo kubwa kisoka duniani. Miaka ya 1990 mchezaji huyo alikuwa ndiye namba tisa hataro zaidi kuweza kutokea duniani katika miaka ya hivi karibuni.

Garrincha

Katika mechi ya mwaka 1985 kati yao na Sweden, alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliochangia kwa kiwango kikubwa kupatikana na ubingwa huo. Alikuwa ni miongoni mwa Wabrazil ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira katika hali yenye kumuudhi mpinzani wake.

Zico

Mchezaji ambaye amefanya makubwa sana na klabu ya Flamengo kwa kuipa vikombe vyenye heshima kubwa duniani na kuijengea heshima klabu hiyo na taifa hilo kwa ujumla. Uwezo wake wa kupiga pasi ulikuwa ni hatari sana hata alipokuwa ndani ya mechi kubwa. Alikuwa anacheza kwa kuamini kwamba kuna wachezaji wanahitaji mipira ya namna gani kushinda.

Ronaldinho

Hiki huwezi kubali kirahisi kwamba jina gani linamfaa mchezaji huyo. Alikuwa na uwezo wa kupiga chenga na kila aina ya udambwiudambwi ambao uliwafanya watu wengi waweze kupenda kuuangalia mpira na kuvutiwa sana kuufuatilia kutokana na kile alichokuwa anakifanya uwanjani kwa wapinzani.

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa