Mwezi Aprili unaendelea kuwa ni mwezi uliojawa na matukio mbalimbali ya kimichezo kote duniani. Wanamichezo wamedhamiria kugoma kutumia mitandao ya kijamii kwa siku 4.

Mgomo huu ambao unaongezewa nguvu na vilabu vya michezo mbalimbali, unashinikiza wamiliki wa mitandao ya kijamii kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya ubaguzi na ukatili unaoendelea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kwa siku za hivi karibuni, kumekuwa na vitendo vya kibaguzi vinavyoelekezwa kwa wanamichezo na makocha wa vilabu mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa timu hizo. Sio kwa wachezaji na makocha pekee, bali hata miongoni mwa mashabiki wenyewe kwa wenyewe, hali ambayo inahatarisha maisha ya baadhi ya waathirika.

Thierry Henry alianza kwa kujiondoa kwenye mitandao yote ya kijamii akidai kuwa, ishara ya kupiga goti kabla ya mchezo pekee yake haitoshi kuonesha upinzani dhidi ya vitendo vya kikatili, badala yake wanamichezo wote wanapaswa kuwawajibisha wamiliki wa mitandao ya kijamii kwani wao wanauwezo mkubwa wa kushughulika na watu wote wanaofanya vitendo hivyo.

Wanamichezo, Wanamichezo Kugoma Kutumia Mitandao ya Kijamii., Meridianbet
Thierry Henry

Mwenyekiti wa Kick Out, Sanjay Bhandari amenukuliwa akisema “mgomo huo unaonesha kukasirishwa kwetu. Kwa kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii, ni ishara kwa wote wenye maamuzi. Tunahitaji mchukue hatua. Tunataka muwesehemu ya mabadiliko.”

Mgomo huu utaanza leo saa 11 jioni mpaka siku ya Jumatatu usiku. Miongoni mwa wanaoshiriki kugoma dhidi ya Twitter, Instagram na FaceBook ni vilabu vyote vya EPL, EFL, Ligi ya Wanawake, Ligi soka nchini Scotland, Mamlaka za FA, Scottish FA, Wales FA, Uefa na vilabu vingine.

Sambamba na wanamichezo, timu na mamlaka za mchezo wa Kriketi, Rugby na Wadhamini mbalimbali kama Barclays na Adidas sambamba na vituo vya matangazo kama vile SkySports, BT Sports na Talksport pia watashiriki mgomo huo.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa