Soka siyo kushuhudia magoli tu namna yanavyofungwa nyavuni, inachangia na ule ufundi unaooneshwa na wachezaji uwanjani ili kuyapata magoli hayo, na hapo ndipo tunasema mchezaji fulani amekamilika na anafaa kuitumikia klabu fulani kubwa. Watu kama Lionel Messi, Ronaldinho, Diego Maradona, Johan Cruyff, Pele, George Best, Garrincha, Ronaldo Luís Nazário de Lima, Okocha na Zidane ni watu ambao ni hatari mno katika sekta hii.

Neymar Jr

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona anatisha sana akiwa na mpira na ni jitihada kubwa sana inahitajika kuweza kuweza kumkaba iki uweze kuumiliki mpira kutoka kwake; wachezaji wengi wamekuwa wakijaribu tu kumchezea mpira wa nguvu ili waweze kumkaba kutokana na maudhi aliyonayo akiwa na mpira uwanjani.

Hatem Ben Arfa

Rennes walikuwa na ingizo hilo katika nafasi hiyo kwa kuonekana kuipa uhai timu hiyo katika msimu huu. Aliifungia timu hiyo magoli na kuchangia upatikanaji wa magoli mengi katika mechi alizozicheza. Alikuwa hatari sana akiwa uwanjani kwa nafasi ya kuuchezea mpira.

Adnan Januzaj

Mchezaji huyo aliyewahi kuhudumu na United ameingia kwenye rekodi hiyo kwa kuwa mchezaji msumbufu sana anayeweza kuuchezea mpira kwa namna ya pekee sana akwa uwanjani. Japo hajawa na msimu mzuri ila amepata kufanya vizuri katika mechi kadhaa anazozicheza.

Lionel Messi

Ni wa La Liga. Amekuwa kwenye ubora wake msimu huu kwa kuweza kufunga magoli kibao ndani ya ligi hiyo. Anakaa katika historia nyingine ya kuwa wachezeaji maridadi wa kabumbu wakiwa uwanjani kwa kuwafanya wapinzani kuwaogopa wakati mwingine, kutokana na uwezo wao.

Youcef Atal

Raia huyo wa Nigeria alikuwa hatari katika ukuta wa Nice kwa kufanya makubwa sana uwanjani. Uwezo wake wa kuuchezea mpira unawafanya makubwa wengi barani Ulaya kuanza kumvizia kutaka kuhitaji huduma yake.

Hazard

Siyo rahisi kucheza na Hazard na kujaribu kuuchukua mpira kwake kama hujajipanga. Alikuwa ni mchezaji wa pekee katika ligi ya Uingereza kutokana na uwezo wake wa kuuchezea mpira na kuwapa majukumu mazito walinzi wa timu pinzani kumzuia.

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa