Bara la Afrika limekuwa na wafungaji mabao mahiri sana tangu enzi na enzi katika ligi mbalimbali duniani kote. Hata hivyo, kuna waliotisha zaidi ya wengine wote. Angalia hapa chini kuwafahamu: 

Samuel Eto’o 

Mchezaji huyo kutoka Cameroon hawezi kupingwa juu ya ubora wake kama mshambuliaji. Alitwaa mataji mawili huko Ulaya, Serie A na mataji matatu ya La Liga yanayomfanya awe ni mchezaji mwenye mafanikio sana duniani.

Umuhimu wake ndani ya bara la Afrika hauwezi kulinganishwa na yeyote yule hata kidogo. Yeye ni mchezaji wa kwanza kushinda mataji mara mbili ndani ya misimu miwili. Ukiachilia ishu ya kushinda taji la UCL mara tatu, La Liga mara tatu na Scudetto, Eto’o anafahamika pia kwa kushinda tuzo ya Pichichi (La Liga Golden Boot) mwaka 2006.

Zaidi ya hayo, yeye ni mfungaji bora wa muda wote wa Africa Cup of Nations’ (AFCON) akiwa na jumla ya mabao 18, ameshinda tuzo ya Golden Boot mara mbili na vilevile ameshinda mataji mawili ya AFCON. Anashikilia rekodi ya Indomitable Lions katika ufungaji magoli. Ukiongezea hapo ni kwamba rekodi ya RCD Mallorca ya kufunga mabao mengi bado anaishikilia yeye mpaka sasa ingawa alicheza kwa misimu minne pekee akiwa pale kwao.

Didier Drogba

Ukilinganisha huyu jamaa na Eto’o, utaona kwamba yeye Drogba amekuwa na mafanikio kadhaa tu kimataifa. Hata hivyo, aliweza kulipaisha sana jina lake na kufanikiwa kuwa ni mmoja ya washambuliaji bora sana wa Kiafrika.

Aliiwakilisha nchi ya Ivory Coast mara tatu kwenye michuano ya World Cup. Alikuwa na mafanikio kwenye AFCON ambako aliweza kuwa mshindi wa ufungaji bora mwaka 2012 na akawa na rekodi kubwa ya ufungaji kwa Elephants.

Tukiachana na hayo yote, mafanikio yake akiwa pale Chelsea yalimpaisha sana katika soka la kimataifa. Aliipeleka Chelsea kutwaa taji lao la pekee la Champions League mwaka 2012. Wakati akiwa kule London alishinda mataji manne ya Premier League, manne ya FA Cups na matatu ya League Cups. Bado anaheshimika kuwa ndiye mshambuliaji mkubwa sana katika klabu ya soka ya The Blues.

Itaendelea…

35 MAONI

  1. Samuel eto’o Umuhimu wake ndani ya bara la Afrika hauwezi kulinganishwa na yeyote yule hata kidogo# meridianbettz

  2. Mungu katujaaria sana africa tuna vipaji vya kutosha na asnte meridian kwa kunijuza na hili pia sikulijua hapo kabla

  3. Makala nzuri kwani inatupa fursa ya kujua mabalaa ya Waafrika katika ligi mbalimbali, tunasubiri toleo lijalo tuzidi kufahamu historia zaidi.

  4. Drogba amekuwa na mafanikio makubwa ngazi yataifa na klabu. Hata hivyo, aliweza kulipaisha jina lake na kufanikiwa kuwa ni mmoja ya washambuliaji bora wa Kiafrika.#meridianbettz

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa