Baada ya Dean Smith kushinda gemu yake ya kwanza akiwa kibaruani dhidi ya Swansea City, Aston Villa walipoteza gemu nyingine dhidi ya Norwich City katikati ya wiki. Wakiwa nafasi ya 16 kwenye msimamo watakuwa wanatafuta kupata ushindi dhidi ya wenyeji wao QPR.
Villa wameshinda gemu 5 tu kati ya gemu 16 walizocheza kwenye michuano yote msimu huu, wamepoteza gemu 5, na kutoa sare gemu 6 ukiwa ni mwanzo mgumu sana wa msimu wao.
Kwa Upande wa QPR, wao hawajachapika katika gemu zao 4 za mwisho, katika hizo 3 wameshinda moja ni sare. Walipata ushindi mkubwa dhidi ya Sheffield wakiwa wenyeji Jumatano kwa bao 3-0. Wanaweza wakapanda nafasi ya saba kama wakipata ushindi leo.
Uso kwa Uso
Hii inakuwa ni mara ya 58 kwa timu hizi kumenyana, QPR wamefanikiwa kucheza gemu 24, Aston Villa wao wameshinda gemu 21 na wametoa sare gemu 13.
Vikosi
QPR XI: | Lumley; Rangel, Leistner, Lynch, Bidwell; Luongo, Cameron; Wszolek, Eze, Freeman; Hemed |
Aston Villa XI: | Nyland; Hutton, Tuanzebe, Chester, Taylor; Hourihane, Whelan, McGinn; Elmohamady, Abraham, Grealish. |
Asha mvugalo
Majanga
isha
Pole sana kwa Aston villa
Povel
Duh majanga kwl
Fatina mfingi
Mmh hatar